Tuesday 12 May 2015

CALL FOR INTERVIEW - KUITWA KWENYE USAILI - 18-22 MAY, 2015

KUITWA KWENYE USAILI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba  Wizara, Idara
zinazojitegemea  na  Wakala  za  Serikali  (MDAs)  anatarajia  kuendesha  usaili  na
hatimaye kuwapangia vituo vya kazi, waombaji kazi watakaofaulu usaili.

Wasailiwa walioitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia

yafuatayo:
1. Usaili utaanza saa moja kamili asubuhi (1:00) na utafanyika mahali na tarehe
kama inavyoonesha katika nafasi husika.
2. Kuja na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi mfano: kitambulisho c ha mkazi,
kupigia kura, kazi, hati ya kusafiria n.k
3. Kuja na Vyeti Halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne, sita,
Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa
za mwombaji.
4. “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato  cha  nne  na  sita  (FORM  IV  AND  FORM  VI  RESULTS  SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
5.  Kila msailiwa aje na picha moja (Passport size).
6.  Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.
7.  Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanyiwa usaili
8.  Kila msailiwa aje na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate)
9.    Kwa wale waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa
na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU & NECTA)
10. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa
maombi yao hayakufanikiwa na wasisite kuomba tena mara nafasi za kazi
zitakapotangazwa.

Tangazo la kuitwa kwenye Usaili-18-22 Mei, 2015
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive