Friday, 1 May 2015

AJIRA MANISPAA YA ILALA - 30/04/2015

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala anapenda kuwatangazia nafasi za kazi Watanzania wenye sifa kama ifuatavyo:-

1.  MTENDAJI WA MTAA III – NAFASI 30
SIFA
Kuajiriwa mwenye Elimu ya Kidato cha IV au VI aliyehitimu Astashahada (CHETI) katika fani ya Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
 KAZI YA MAJUKUMU
i.                    Katibu wa Kamati ya Mtaa
ii.                  Mtendaji Mkuu wa Mtaa
iii.                Mratibu wa utekelezaji wa Sera na Sheria zinazotekelezwa na Halmashauri katika Mtaa
iv.                Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu Mipango ya Maendeleo katika Mtaa
v.                  Msimamizi wa Utekelezaji wa Sheria Ndogo pamoja na Sheria nyingine zinazotumika katika Mtaa.
vi.                Mshauri wa Kamati ya Mtaa kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama
vii.              Msimamizi wa utekelezaji wa mikakati mbalimbali inayohusu uondoaji wa njaa na Umaskini katika Mtaa;
viii.            Kusimamia ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri na kutunza kumbukumbu za walipa kodi wote;
ix.                Kuandaa na kutunza rejesta ya wakazi wote wa Mtaa na
x.                  Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
NGAZI YA MSHAHARA –  TGS. B


MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU II – NAFASI II – NAFASI 10

SIFA:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV/VI wenye cheti cha Utunzaji Kumbukumbu kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.

KAZI NA MAJUKUMU
Wasaidizi wa kumbukumbu watafanya kazi zifuatazo hapa chini kwa kuzingatia fani walizosomea na kazi wanazofanya ni kama vile Uhifadhi wa Nyaraka, Uhifadhi wa Kumbukumbu za Afya, Ardhi na Masjala ya Kawaida,

1          KAZI YA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA II

Daraja hili la mafunzo katika kazi, hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya wasaidizi wa kumbukumbu walio juu yake. Kazi atakazojifunza na kufanya ni zile zifanywazo na Msaidizi wa Kumbukumbu daraja la I.
2.         KAZI ZA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA I
            i.          Kutafuta kumbukumbu/nyaraka/mafaili yanayohitajiwa na wasomaji
            ii.         Kudhibiti upokeaji, uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
            iii.        Kuchambua, kuoredhesha na kupanga kumbukumbu/nyaraka katika makundi
kulingana na somo husika (classification and boxing) kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
            iv.        Kuweka/kupanga kumbukumbu/nyaraka katika reki (file racks/cabinets) katika
masjala/vyumba vya kuhifadhia kumbukumbu.
            v.         Kuweka kumbukumbu (barua, nyaraka n.k) katika mafaili.
            vi.        Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
                     
NGAZI YA MSHAHARA – TGS. B
MASHARTI YA JUMLA
 Mwombaji lazima awe Raia wa Tanzania
Awe amehitimu na kupata Cheti cha Taaluma cha Kidato cha Nne (IV) NB. Results Slip hazikubaliki.
Awe na Cheti cha Kuzaliwa
Barua zote ziambatane na nyaraka zifuatazo:-
i.                    Nakala za Vyeti vya Mwombaji vilivyothibitishwa,
ii.                  Maelezo binafsi ya Mwombaji (Curriculum Vitae),
iii.                Picha ndogo za rangi (Coloured Passport size) mbili (2) za Mwombaji za hivi karibuni.
Kila Mwombaji lazima awe na Umri kati ya miaka 18 – 45
Waombaji wenye sifa Pungufu au Zaidi na zilizotajwa hapo juu hawashauriwi kuomba kwani maombi yao hayatafanyiwa kazi.
Watumishi waliopunguza kazi/kufukuzwa kazi Serikali hawashauriwi  kuomba
Waombaji ambao wameajiriwa wanashauriwa kupitishia barua zao za maombi kwa waajiri wao wa sasa.
Barua ambazo hazikuambatishwa na nyaraka zilizotajwa hapo juu (i–iii) hazitashughulikiwa.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono, zikiwa na  anwani kamili ya Mwombaji, pamoja na namba ya simu na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

MKURUGENZI WA MANISPAA
MANISPAA YA ILALA
S. L. P 20950
DAR ES SALAAM.

TAREHE YA MWISHO YA KUPOKEA MAOMBI:-
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 14/05/2015 saa 9:30 Alasiri

Tangazo hili linapatikana pia kwenye Blog ya Manispaa ya Ilala – www.habariilala.blogspot .com

Limetolewa na;

ISAYA M. MNGURUMI
MKURUGENZI WA MANISPAA,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA

Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive