Friday 8 May 2015

TANGAZO LA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA BUMBULI - 07/05/2015

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli kwa mujibu wa Kibali cha Ajira mpya chenye Kumb. Na. CB.170/369/01/H/138 cha tarehe 23/04/2015 taka kwa Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa Umma, anatangaza nafasi zifuatazo za ajira kwa watanzania wote wenye sifa na wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 45.

1. KAZI YA Katibu Mahsusi Daraja La III- TGS. B ( NAFASI 5)
A) Sifa za waombaji:
i.Wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria mafunzo yo Uhazili na kufaulu mtihani
wa Hatua yo Tatu,
ii. wawe wamefaulu soma la Hati Mkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 80
kwa dakika moja.
Iii. wawe wamepata mafunzo ya Kompyuta kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali na kupata Cheti katika programu za
Windows,Microsoft Office, Internet, E-mail na Publisher.

B) Kazi za kufanya:
i. Kuchapa boruo. taarifa na nyaraka za kawaida.
Ii. Kusaidia kutafuta na kumpatia mkuu wake majalada no nyaraka zitakazo hitajika katika shughuli zokozi Ofisini. .
iii. Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
IV. Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa maafisa no kuyakusanya, kuyatunza no kuyarudisha sehemu zinazohusika.
v.Kutekeleza kazi zozate atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa
kazi.

KAZI Ya Msaidizi Wa Kumbukumbu Daraja la II-TGS. B (NAFASI4)

A) Sifa za waombajl:
i. Waombaji wawe wamehitimu kidato cha IV au kidato cha VI.
ii. Wawe na Cheti cha Utunzaji wa Kumbukumbu katika moja wapo ya Fani za
Afya, Masjala na Ardhi.

B) Kazi za kufanya:
i. Kutafuta nyaraka/majalada yanayohitajiwa na wasomaji.
ii. Kudhibiti upokeaji na uandikishaji wa kumbukumbu/nyaraka.
Iii. Kuweka barua/nyaraka katika majalada .
iv. Kushughulikia maombi ya kumbukumbu/nyaraka kutoka Taasisi za Serikali.
v.Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na msimamizi wake wa kazi.

Afisa Mtendaji Wa Kijiji Daraja La III-TGS. B (X 24)
A) Sifa za waombajl:
i. Waombaji wawe wamehitimu kidato cha IV au kidato cha VI.
Ii. Wawe na Astashahada/Cheti katika moja wapo ya fani zifuatazo:-
Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii (Socia logy) , Usimamizi wa Fedha (Financial
Management), Maendeleo ya jamii (Community Development) na Sayansi
yo Sanaa (Social Work) kutoka katika Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.
Dodoma au Chuo chochote kinachotambuliwa no Serikali.

B) Kazl za kufanya:
i. Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji.
Ii. Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Hi. Msimamizi wa Utawala bora katika Kijiji.
IV. Kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo Kijijini. .
v.Katibu wa mikutano na kamati zote za Halmashauri ya Kijiji.
vi. Kutafsiri na kusirnornio Sera, Sheria na Taratibu.
vii. Kusimamia. kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nyaraka za Kijiji.

APPLICATION INSTRUCTIONS:

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE

Maombi vote yatumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji. Halmashauri ya Bumbuli.
S.L.P. 111. BUMBULI.

Maombi vote yaambatane na vivuli vya vyeti vya taaluma. mafunzo no vyeti
vya kuzaliwa vilivyothibitishwa na Mahakama au na mtu yeyote aliyeidhinishwa.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (CV) yenye anwani
na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yo wadhamini wa tatu wa kuaminika.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 22/05/2015 saa 9:30 Alaslrl.
Maombi vote yatumwe kupitia Posta kwa anuani tajwa hapo juu.
Waombaji waliopita (shortlisted) ndiyo watakaotaarifiwa kwa ajili ya kuja
kufanya usaili.

Tangazo hili limetolewa na;
Beatrice K. Msomisi
MKURUGENZI MTENDAJI
HALMASHAURI YA BUMBULI
Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive