Thursday 7 May 2015

KUHUSU UJAZAJI WA TAARIFA SAHIHI KWENYE MFUMO WA RECRUITMENT PORTAL

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika utumishi wa Umma, Bwana Xavier Daudi, anaendelea kuwasisitiza waombaji kazi kuwa wahakikishe wanaingiza taarifa zao hususan za kitaaluma kwa uhakika na kufuata maelekezo yanayotolewa kwa kila tangazo la kazi husika. Pia Daudi amesisitiza kuwa barua ya maombi ya kazi inapaswa kuambatishwa kwenye sehemu uliyoandikwa other attachments na taarifa zingine ziambatanishwe kwenye kila kipengele kadri zilivyogawanywa kwenye mfumo huo.

Daudi ameongeza kuwa kwa muombaji kazi ambaye atatuma maombi ya kazi kwa kutumia mfumo wa Recruitment Portal bila kujaza taarifa zake kwa ufasaha atambue kuwa maombi yake hayatakubaliwa.

Aidha waombaji kazi ambao bado hawajajisajili kwenye mfumo huo wanashauriwa kufanya hivyo kwa kufungua http://portal.ajira.go.tz ili waweze kuingiza taarifa zao ambazo zitawasaidia wakati wowote nafasi za kazi zitakapokuwa zikitangazwa kutuma maombi yao kupitia mfumo huo.

Mwisho, waombaji kazi wote ambao waliwasilisha maombi yao ya kazi kupitia mfumo wa Recruitment Portal maombi yao yanaendelea kuchambuliwa na mara baada ya mchakato huo kukamilishwa, watakaokuwa wameitwa kwenye usaili watafahamishwa kupitia tovuti ya Sekretarieti ya ajira.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasilaino Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. 6 Mei, 2015.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo 0687 624 975 au 0784398259

Share:

0 comments:

Post a Comment

Blog Archive